THINGS I WISH MY 15-YEAR-OLD SELF KNEW featuring Mary Owendi
2nd December 2022On creativity:
Hey little Owendi, to be honest mama you’ve got to be you na hata kama ni kumake tiktok videos, dancing, singing au acting, you have to do it juu at the end of the day wewe ndio unajua nini unataka kwa life yako.
On school:
Najua shule inakuanga na pressure mob but honestly education ndio itakuhelp huku nje. Na lazima uwork hard ndio ujimake proud na pia parents wako. All the best siz!
On friends:
Friends, friends…babe this is the time ya kumake friends. Make as many friends as possible and learn from them, but be careful na friends unachoose because si unajua ile saying ya Show me your friends and I’ll tell you wh0 you are.
On fashion:
Nani hapendi kukaa poa? Definitely kila mtu anapenda kukaa vizuri tena sana. So ukichagua outfit ya kuenda place usifeel ati ooo siko worth it…ooo sikai poa…as long as you are comfortable and looking beautiful wewe jibambe!
On failure:
Kwa hii life hakuna kitu kama failure na ukiona kitu haiwork for you usigive up, keep on trying and trying and at the end of the day itakuja kuwork in your favour. Ukifall, wake up, dust yourself up na umove on to the next level of life. Hakuna kugive up!
On boys:
Ladies! Si kila boy ni msee mbaya but always know the way to sway around them and how to stay true to yourself. Usijisahau juu ya pressere kutoka maboys. Ukona the choice kuamua kama unataka kudate ama kungoja, usijipatia stress kufanya kenye watu wengine wanafanya, unadeserve kuchoose what you want for yourself. Choice ni yako!
On peer pressure:
Baby girl! Hufai kupressuriwa kufanya kitu hutaki. You have the right to say no to negative vibes or energy. Usiwache msee akuforce kusmoke vitu kama shisha na cigarettes juu ziko na tobacco na sio a cool thing to do. Ukiona beshte anakuletea hizo stuff wewe sema zii juu it’s not your thing!
On the future:
I know kila mtu anataka kuwa na future poa. Kitu utado ni kufocus on your life na kukeep God mbele kwa kila kitu juu yeye ndio atakuguide. You got this siz!
On doing what you love:
If you love something lazima utie-bidii na uifanye na roho yako yote juu hio talent itakuja kukuhelp baadaye. So just focus on what you love na kumbuka udeserve kumake choices zako mwenye.