Take The Pledge Today

Piga Looku: Tuchambue Hizi Trends

8th August 2025

Wah babe, wacha tu! Trends zinakam na zikienda kama mat za Ngong Road, lakini style ni forever. Na recently, SKY Girls wako on fire wakimix past na present hadi inabamba!

Let’s break it down, zile old-school styles kutoka kitambo, na venye madem wanaziremix saa hii:

Mum Jeans 2.0


Remember zile wide-legged jeans aunties walikuwa wanaslay nazo kwa 90s? Zimerudi na sasa ni glow-up! Madem sahi wanaziremix na crop tops, thrifted jackets, vintage shades na chunky sneakers. Ni kama kupea nguo za mzae life mpya!

Hair Vibes: Retro Meets Right Now


Bantu knots na box braids zimeupgrade! Sasa ni colours na beads, na ka-baby hair laid kidesign. Ni kama kila hairstyle ina-story yake. Sharon, 17, alituambia: "Nikiweka braids na beads, najifeel powerful but still looking cute." Hiyo ndio vibe

Bold Lipstick & Eyeshadow


Kitambo, makeup kit ilikuwa na classic red lipstick na blue eyeshadow combo – hii niko sure umeona hadi kwa movies za Afro sinema. Sahi ni glossy lips, colored liners, na graphic eyes. Still bold, but more us!